AFANDE SELE AJIUNGA RASMI NA CHADEMA

Rasmi jana Jumapili msanii maarufu wa hip hop, Afande Sele amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Afande ameonyesha ni mwenye furaha na kwenye mtandao wa Facebook ameweka maneno haya.
Hakuna kusanda,hakuna kumbwanda,mbele kwa mbele makamanda,vua gamba vaa gwanda kisha kaza mkanda, wanashuka sisi tunapandaaa,,,,Leo tunaanza kuandika hisyoria mpya ktk mkoa wetu wa morogoro na tz kwa ujumla kwa sababu nikiwa kama msanii wa muda mrefu na mfalme pekee wa mzk wa kizazi kipya ninaetunga nyimbo zangu kwa kuzingatia ujumbe muhimu ktk jamii kwa mambo ya kisiasa,kiuchumi,elimu,amani na upendo nk,sasa leo nimeamua kwa ridhaa yangu iliyosukumwa na uzalendo na mapenz makubwa kwa taifa langu kuchukua kadi ya kujiunga rasmi uanachama wa CHADEMA,tukio hilo kubwa litafanyika leo jioni ktk mkutano wa hadhara utakaofanyika kata yetu ya mafiga/misufini na utahudhuriwa na viongoz mbalimbali wa chama kutoka makao makuu ya chama dsm pamoja na mbunge wa nyamagana mh ezekiel wenje,kwa wakaz wa moro wazalendo nyote mnakaribishwa saaana,ahsanteni wana'ndugu,siasa si uadui,tupingane/tusipigane,Pendo moja!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post