Hatimaye
kituo cha afya Kalumwa kilichopo katika wilaya mpya ya Nyang’hwale mkoani Geita kimeanza
kupata neema ambapo leo kimeahidiwa kupatiwa magodoro 50 na vitanda 2 vya kujifungulia
akina mama vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3 na laki tano.
Ahadi hiyo imetolewa
leo na Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale mheshimiwa
Hussein Nasoro Kassu baada ya kutembelea kituo hicho na kijionea hali halisi ya
kituo hicho na kutoa msaada midogo midogo kwa wagonjwa waliolazwa katika kituo
hicho vikiwa na thamani ya shilingi laki moja na elfu kumi.
Mbunge juyo
amesema ameamua kutoa misaada na ahadi
hiyo ya magodoro 50 na vitanda 2 baada ya kujionea mwenyewe wagonjwa wa jimbo lake wanavyoteseka
huku akina mama wakiwa hawana vitanda maalumu vya kujifungulia huku mazingira
ya vyoo na mabafu yakiwa machafu.
Aidha kufuatia
ziara hiyo ya kushutukiza ya mbunge huyo wa Nyang’hwale ameiomba halmashauri hiyo
kutafuta njia mbadala ya kukisaidia
kituo hicho ambacho wagonjwa wake wana hali mbaya huku wakisubiri pesa kutoka serikali
kuu.
Naye Mganga
mkuu wa kituo hicho DK Nelson Bukuru pamoja na wagonjwa waliokutwa katika kituo
hicho wameshukuru sana kwa msaada wa mbunge huyo
na kumuomba kuendelea kuwasaidia na kuwaomba wahisani wengine wenye moyo kama wa mbunge kuendelea kukisaidia kituo hicho,
Ziara ya
mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale mheshimiwa
Hussein Nasoro Kassu katika kituo hicho cha afya imekuja ikiwa ni siku chache
tu mtandao huu wa www.malunde1.blogspot.com
kuripoti kuhusu hali mbaya katika kituo cha afya cha Kalumwa kilichopo katika
wilaya mpya ya Nyang’hwale mkoani Geita.
Social Plugin