HATARI SANA--!!!! JAMAA AKATWA NYETI ZAKE AKIWA AMELALA KWA SHEMEJI YAKE

NB-Siyo picha ya Mwami Mwanalusi  
Mtu mmoja Mkazi wa Kijiji cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Mwami Mwanalusi (31) amekatwa na kisu katika sehemu zake za siri na watu wasiojulikana wakati akiwa amelala ndani ya nyumba ya shemeji yake na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi wa  Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa nane usiku nyumbani kwa shemeji yake.

Alisema siku ya tukio  Mwami  alikuwa amekwenda  kumtembelea  shemeji yake aitwaye  Anset  Kapampala (36) ambae alikuwa akiishi katika kijiji hicho cha Majimoto.

Baada ya mlo wa usiku mwenyeji wake alimwonesha chumba cha kulala ambacho hata hivyo hakikuwa na godoro wala kitanda bali kulikuwa na Benchi la kupumzikia ambalo shemeji yake ambae ni mwenyeji wake alimweleza Benchi hilo ndilo alitumie kama kitanda cha kulalia kutokana na hali yake ya kiuchumi kutokuwa nzuri.

Alisema wakati Mwami yuko ndani ghafla walitokea watu asiowafahamu ambao waliingia ndani ya chumba hicho  na wala hawakumsemesha chochote hali ambayo ilimfanya ashikwe na butwaa.

Alieleza ndipo watu hao walipoanza kumkata kwa kisu sehemu zake za uume hadi uume wake ukawa umeharibika vibaya  na kisha watu hao wakatokomea kusikojulikana  na kumfaya yeye apige mayowe  ambapo shemeji yake  ambae alikuwa amelala kwenye nyumba yake nyingine  alishtuka na ndipo alipoingia ndani na kumkuta mgeni wake akiwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za siri.

Kamanda Kidavashari alisema chanzo cha tukio hilo  bado hakijulikana  na polisi wanaendelea na upelelezi ili kuwabaini  na kuwakamata waliohusika ili sheria  ichukuwe mkondo wake. 
Chanzo-katavi yetu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post