Imetokea huko Amerika Dada mmoja anayeitwa Apryl Michelle Brown, ambaye alienda kuchoma sindano ya kuongeza makalio kwenye kituo fulani cha urembo na afya huko marekani alifanya hivyo kwakuwa hakuwa ameridhika na ukubwa wa makalio yake na kufanya uamuzi wa kutafuta mbinu ya kuyaongeza.
Dada huyo baada tu ya kuchoma sindano hiyo alikaa mwezi mmoja nakuanza kupata maumivu makali kwenye miguu yote miwili na mikono.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi na ilibainika kuwa sindano aliyochoma haikuwa sahihi na matokeo yake ilisababisha sumu mwilini, ambapo wataalamu walisema kuwa sindano hizo huchomwa kulingana na Mwili wa mtu pia aina na uwezo wa chembe chembe zake za damu.
Inasemakana aliyechoma hakuangalia ni aina gani ya sindano ambayo ingeweza kuendana na mwili wa dada huyo.
Hivyo kumpelekea dada huyo kutopata nafuu na badae wataalamu kuamua kumkata Mikono yake na miguu.
Dada huyo alivieleza vyombo vya habari kuwa " nitajutia maisha yangu yote kwa jambo nililo fanya".
INASIKITISHA: WAKIDADA HILI NI FUNZO KWENU..!!
chanzo-clicktz
Social Plugin