KANISA KATOLIKI LEO LINAADHIMISHA MWAKA 1 WA KIFO CHA ALIYEKUWA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI JIMBO LA SHINYANGA MHASHAMU ASKOFU ALOYSIUS BALINA
Wednesday, November 06, 2013
Askofu Balina Enzi za uhai wake
Waziri
Mkuu, akiwa na Askofu Balina katika Ibada ya kumsimika Askofu wa Jimbo la Bunda
iliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Katoliki Parokia ya Bunda
Februari 20, 2011.
Leo kanisa kanisa katoliki linaadhimisha mwaka mmoja tangu
kufariki dunia kwa aliyekuwa askofu wa jimbo katoliki la shinyanga mhashamu
Aloysius Balina amabye alifariki dunia tarehe 6 mwezi Novemba mwaka jana majira
ya saa tano asubuhi katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa anatibiwa
ugonjwa wa saratani ya ini.
Mazishi yake yalifanyika tarehe 11 Novemba mwaka jana katika
kanisa la Mama mwenye Huruma lililoko Ngokolo mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
dini,vyama vya siasa na serikali akiwemo rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Marehemu Askofu Balina alizaliwa mwezi Juni 21 mwaka 1954
huko Isoso wilaya ya Bariadi mkoa mpya wa Simiyu,akapewa daraja takatifu ya
upadre Juni 27 mwaka 1971 na mwaka 1984 akateuliwa kuwa askofu wa kwanza wa
jimbo Katoliki la Geita na Baba Mtakatifu Papa Paulo wa pili.
Alisimkwa rasmi kuwa askofu wa jimbo katoliki la Geita
Januari 6 mwaka 1985 na baadaye mwaka 1997 aliteuliwa kuwa askofu wa jimbo
katoliki la Shinyanga kufuatia kifo cha aliyekuwa askofu wa jimbo la Shinyanga
marehemu Castory Sekwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka jimbo katoliki la Shinyanga misa ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha Askofu Balina itafanyika leo majira ya saa kumi na nusu katika kanisa la Mama mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA MBINGUNI ROHO YA MAREHEMU ASKOFU BALINA.Amina!
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin