WAUGUZI WATUHUMIWA KUTUKANA WAGOJWA KITUO CHA AFYA KALUMWA WILAYA MPYA YA NYANG'HWALE- GEITA

NB-Picha siyo ya kituo cha afya cha Kalumwa


Na Valence Robert ,Nyang’hwale (Geita)

Wagonjwa  waliolazwa katika kituo cha afya Kalumwa kilichopo katika wilaya mpya ya Nyang’hwale mkoani Geita wako hatari kupoteza maisha yao kutokana na huduma za matibabu zinatolewa na wauguzi waliopo kuwa mbovu na ambapo pia wagonjwa wamekuwa wakitukanwa na wauguzi.

Hayo yamebainika leo  baada ya  ya waandishi  wa habari kutembelea  kituo hicho ambapo wagonjwa hao wamesema  kituo hicho kinatoa huduma mbovu huku wakiongeza kuwa  vitendo vya rushwa vimekithiri kwa wauguzi hao na kama huna pesa unakufa huku ukijiona.

Wameongeza kuwa kutokana na wauguzi kutotoa huduma bora na kuwatukana wagonjwa bado kuna changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho kama vile ukosefu wa vyoo ,maji ,umeme na dawa vitanda pamoja na magodoro.

Wamesema kutokana na suala la usafi kutopewa kipaumbele sasa hivi wadudu aina ya kunguni ambao wamekuwa kero kwa  wagonjwa hali inayosababisha pia kuambukizwa magonjwa mengine.

“Waandishi sisi wagonjwa tunashangaa hakuna vyoo mpaka tunakosa sehemu ya kujisaidia ,dawa hata panado hakuna mpaka ununue, kama huna pesa unakufa”,alisema mgonjwa mmoja ambaye akutaka jina lake litajwe.

Hata hivyo alipotafutwa na waandishi wa habari  kwa njia ya simu mkononi kutokana na kutokuwepo ofisini kwake mganga mkuu wa wilaya hiyo Dk .Nelson Bukuru ili kuzungumzia matatizo hayo amesema kuwa bado wilaya ni mpya lakini matatzo yote anayajua na anayafanyia kazi na kuwaomba wagonjwa kuwa na subira wakati halmashauri ikishugulikia matatizo hayo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post