kesho ni zaidi ya hii |
Ikiwa kesho ni siku ya kisukari duniani katika mkoa wa
Shinyanga maadhimisho ya siku hiyo yataadhimishwa kwa aina yake ambapo
kutafanyika maandamano ya kutembea kwa miguu kutoka eneo la hospitali ya mkoa
wa Shinyanga kupitia maeneo mbalimbali mjini Shinyanga na kuhitimishwa katika
viwanja vya Shy-com ..
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt Ramadhani
Kabala amesema siku ya kisukari duniani hufanyika tarehe 14 mwezi Novemba kila
mwaka kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kujua sababu
zinazosababisha mtu kuwa na ugonjwa wa
kisukari na kwa walio na kisukari kuwapa elimu ya namna ya kukabiliana na
ugonjwa huo.
Dkt Kabala mesema katika maadhimisho hayo ya siku ya
kisukari kesho katika mkoa wa Shinyanga,mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Ally Nassoro
Rufunga ambaye pia ataongoza maandamano ya kutembea kwa miguu
Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataanza kwa maandamano ya
kutembea kwa miguu kwa kasi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi na yataanzia katika
hospitali ya mkoa wa Shinyanga kupitia shule ya Sekondari Buluba iliyoko mjini
Shinyanga kuelekea Stendi ya mabasi mjini Shinyanga kupitia eneo la Japanese
kona hadi Kanisa la AIC Kambarage baadae Nguzo nane na hatimaye kuishia katika
viwanja vya SHY-COM ambapo kiongozi wa maandamano hayo ambaye ni mkuu wa mkoa
wa Shinyanga atatoa hotuba.
Amesema lengo la maandamano ya kutembea kwa miguu kwa kasi
ni kuwahamasisha wananchi kuwa kutembea
kwa miguu ni njia bora na rahisi zaidi ya kufanya mazoezi kwa lengo la
kukabiliana na ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine sugu yasiyoambukizwa
kama vile presha.
Social Plugin