Na John Banda, Dodoma
Nabii Elisha Muliri wa kanisa la Ebeneza mjini hapa
ameingia matatani baada ya kudaiwa kumbaka na kumtia mimba mwanafunzi na
kukatiza masomo yake huku kutishia kumuua.
Akisimulia tukio hilo mbele
ya waandishi wa habari mwanafunzi huyo Martha Daniel [17] kidato cha tatu
katika shule ya sekondari ya City ilyopo manispaa ya Dodoma alisema kabla ya kufanyiwa kitendo
hicho alikuwa anaangushwa na mapepo.
Martha alisema baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila
mafanikio walipata taarifa za ujio wa nabii huyo mjini humo na wapofika ili
kupata msaada wa kuombewa mapepo hayo yalilipuka na binti akaponywa hata leo na
kuahidiwa mbele ya kanisa kusaidiwa ada na Nabii huyo.
Binti huyo alisema baada ya kuponywa akaendelea kwenda
kusali kanisani hapo ambapo kutokana na kila mtu anayefika na kufanyiwa maombi
huacha mawasiliono kwenye vikaratasi, na Juni 8 mwaka huu majira akapigiwa simu
na Nabii huyo akipewa .
maelekezo ya kufika nyuma ya ukumbi wa Paradise
ambapo walikuwa wakifanyia ibada.
Anatanabaisha kuwa baada ya kuonana Nabii alimwambia aingie
kwenye Gari akaingia akifikili kuna heri akapewa soda aina ya Fanta orange
alipokunywa akapoteza fahamu na alipokuja kuzinduka alijikuta akiwa nyumba za
kulala wageni makole na Nabii akiwa amemlalia kama
alivyozali huku akiangalia mkanda wa Ngono.
‘’Wakati nataka kupiga kelele alinitishia kwamba ataniua
kama nitathubutu kumwambia mtu yoyote jambo hilo, akanipiga kofi na kuniambia yeye hawezi
kunilipia ada bure kwa sababu mimi siyo ndugu yake lazima lazima alale na mimi
mara 5 kwa hiyo bado mara 4 na kunisisitiza asisikie popote kuwa alinifanyia
hivyo’’, alisema Mwanafunzi huyo
Kwa upande wake Mama mzazi wa mwanafunzi huyo Mary Mkombora
alisema alimpeleka kuombewa kutokana na kusubuliwa na mapepo tangu akiwa Darasa
la sita na wakakubaliana na Nabii huyo kumlipia ada kwa awamu hivyo akachukue
50,000 kila mwezi ili kukamilisha 400,000 inayotakiwa shule.
Nilimgundua yupo tofauti kuanzia mwezi wa saba nilipomuuliza
alisema yeyue haelewi siku moja nikamshuhudia akitapika asubuhi ndipo
nilipochapa na kumfukuza nikapigiwa simu na waliompokea kua mtoto kapewa mimba
hiyo na Nabii kwanini nimemfukuza ndipo nikachoka, alipopimwa alikuwa na mimba.
Alisema Nabii huyo ambaye alikuwa Mume wa mwimbaji Marufu wa
Nyimbo za Injili marehemu Anjera Chibalonza kwa sasa hajulikani alipo japo mara
kadha wasaidizi wa kanisa hilo ambalo limebadilishwa
jina kutoka Shakinah
Pentecostal Church
na kuitwa Ebeneza wamekuwa akitaka Suruhu.
‘’sasa hivi mimi na mtoto wangu tumekuwa tukiishi
mashakani baada ya Msaidizi wake Nabii Monica nimpe Martha akamtoe mimba
kwa ataaramu anaowajua wao, siku ambayo alichukua kadi yenye namba za simu na
kufuta meseji zote mwanangu alizokuwa akiandikiwa na Nabii,’’
Nabii huyo kwa sasa hajulikani alipo na hata alipotafutwa
kwa simu yake ka mkononi 0756 409118 ilikuwa amezimwa na msaidizi wake Nabii
Monica Nyambura raia wa nchini Kenya anakotoea Elisha Muliri alisema yeye
hawezi kuongelea jambo hilo kwakua yeye ni mgeni ameachiwa kanisa hilo baada ya
mwenyeji wake kuwa safarini hivya asubiliwe hatachelewa.
Tukio hilo
limefikishwa katika kituo cha sheria cha Tanzania Legal Centre [TALAC] na
mwanasheria mfawidhi mkazi Dodoma Godwin Ngongi tayali ameshamuandikia mkuu wa
kituo cha polisi kati barua ya kuwataka kumkamata mtuhumiwa huyo ili afikishwe
kwenye vyombo vya sharia na pia kuepusha mwanfunzi huyo na hatari
nyingine.
Jeshi hilo
limekiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi
Social Plugin