Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya |
Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Masanja Joseph (44) mkazi wa wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa gongo kichwani na Minas Mihangwa mkazi wa
kijiji cha Seseko,kata ya Songwa,tarafa ya Mondo,wilayani Kishapu mkoani
Shinyanga.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya
Kihenya amesema tukio hilo
limetokea juzi saa tatu na nusu usiku katika kijiji cha Seseko kata ya Songwa
tarafa ya Mondo wilayani Kishapu, baada ya marehemu kumfumaniwa na mke wa Minas
Mihangwa.
Kamanda Kihenya amesema chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu
wa kimapenzi na kwamba jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa wa mauaji hayo
Social Plugin