NB-picha haihusiani na tukio |
Kijana mmoja
ambaye hakuweza kufahamika mara moja jina wala makazi yake(28) ameuawa kwa
kushambuliwa kwa kipigo kikali kisha kuchomwa moto baada kumchoma kisu tumboni mwendesha
baiskeli maarufu daladala ili kumwibia baiskeli mwendesha baiskeli huyo.
Tukio hilo
limetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika kitongoji cha Bubalaji kata ya
Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga
ambapo walioshuhudia
tukio wamesema marehemu alikuwa anafanya jaribio la kuiba baiskeli ya mwendesha
daladala ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja.
Kufuatia kuchomwa kisu mwendesha baiskeli huyo alianza kupiga kelele za kuomba msaada na muda mchache watu waliokuwa jirani na eneo la tukio walikusanyika na kumkamata marehemu na kuanza kumshushia kipigo na kisha kumchoma .
“Kijana huyo
kabla ya kifo chake alimkodi mwendesha daladala aliyekuwa na baiskeli katika eneo la Kambarage mjini Shinyanga ili ampeleke
kijiji jirani cha Uzogore lakini walipofika katika mto uliopo eneo la kitongoji
cha Bubalaji kijana alimwamuru mwendesha
daladala huyo asimame na baada ya kusimama alimchoma kisu tumboni na
kutumia nafasi hiyo kuiba baiskeli yake",alieleza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Mwendesha daladala anayesadikiwa kukodiwa na marehemu amekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa matibabu baada ya kuchomwa kisu tumboni na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Social Plugin