MBUNGE ALIYESHINDWA KUTEKELEZA AHADI ZAKE APIGWE CHINI 2015,ASEMA MWENYEKITI MSTAAFU CCM MKOA WA TABORA
Sunday, November 03, 2013
Mwenyekiti
mstaafu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Juma Samwel Nkumba akizungumza na
baadhi ya wananchi wa mjini Tabora kata ya Mtendeni ambapo
alisisitiza kuwa makini wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015,kuchagua
viongozi ambao wapo karibu na wananchi wakisaidia kukabiliana na
changamoto mbalimbali na si kuchagua viongozi hususani Wabunge ambao
hawana muda wa kukaa karibu na wananchi waliowapigia kura na hivyo
kuwataka wawapige chini ambao waliahidi ahadi kibao wakati wa kuomba
kura na mara baada ya kuchaguliwa wamekuwa hawataki kusogea karibu na
wananchi,jambo ambalo limekuwa likishusha heshima ya CCM kwa wapiga
kura.
Mjumbe
wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka
akizungumza katika hafla fupi ya shukrani ya diwani wa kata ya Mtendeni
Bw.Ngalu,...Katika hotuba yake Bw.Mwakasaka alitumia fursa hiyo
kusisitiza juu ya umuhimu wa kukiimarisha CCM kabla na baada ya uchaguzi
jambo ambalo limekuwa likipigwa vita na baadhi ya Viongozi wa CCM
ambao wanashindwa kuwa karibu na wananchi na kufanya mikutano ya mara
kwa mara itakayosaidia kukijenga Chama hicho.Aidha ameongeza kusema kuwa
ni vema wanaCCM wakajenga mazingira ya ushirikiano utakaowawezesha
kuwatumikia wananchi waliokipatia ridhaa chama hicho kuongoza dola
badala ya kuendelea na marumbano yasiyo na tija hasa wakati huu ambao
uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kutekeleza ilani ya chama hicho.
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Abraham maarufu Nkonkota naye
alipata fursa ya kuzungumza katika hafla hiyo ambapo pamoja na mambo
mengine Mwenyekiti huyo alisema kuwa kwasasa Chama hakina nafasi ya
kumuonea aibu kiongozi yeyote aliyeshindwa kutekeleza ahadi zake kwakuwa
jambo hilo litaendelea kukichafua CCM mbele ya wananchi....Nkonkota
aliongeza kuwa nia ya CCM ni kutaka kutoa huduma bora kwa wananchi
waliowachagua na kamwe hakita kubali kumkumbatia kiongozi anayeshindwa
kutekeleza majukumu yake kama alivyoahidi na kubwa zaidi CCM itakuwa
macho kuangalia mtu anayekubalika kwa wananchi na si kuwalazimisha
wachague kiongozi mjanja mjanja wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015
utakapowadia.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin