Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mila ya Ajabu Sana!!!--MAITI WANAFUKULIWA MAKABURINI NA KUBADILISHWA NGUO NA KUTEMBEZWA KIJIJINI- HUKO INDONESIA

Ukisikia maajabu ndiyo haya sasa,kila mwaka huko katika Kisiwa cha Sulawesi, Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo na kuwatembeza kijijini hapo. 

Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila ya ajabu inayoiitwa Ma'nene  ambayo wanaamini mtu akifa bado yuko nao kwa hiyo inawalizimu kufanya mambo hayo kama kuwabadilisha nguo.

Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.

Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.
chanzo-bongonews

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com