Na Valence Robert-Geita
Mkutano mkubwa wa siku mbili wa kukabiliana na wahamiaji haramu pamoja na majambazi wanaotumia Silaha kutoka nchi zinazopakana naTanzania
umeanza kufanyika katika Mkoa wa Geita.
Mkutano mkubwa wa siku mbili wa kukabiliana na wahamiaji haramu pamoja na majambazi wanaotumia Silaha kutoka nchi zinazopakana na
Akifungua
mkutano huo leo katika ukumbi wa Alufa Hotel mjini Geita ,mgeni rasmi Mkuu wa
mkoa wa Geita Magalula Said amesema kuwa
pamoja na kufanya mkutano uwo mafisa uwamijia wa Mikoa wanatakiwa kuwa makini
kwani kuna maafisa ambao si waadilifu katika kazi zao ambao wamekuwa wakipewa pesa na kurudisha nchini
wahamiaji waliorudishwa kwao.
Naye kamishina
utawala wa fedha kutoka makao mkuu Piniel Mgonja kwa niaba ya kamishina mkuu wa
uhamiaji Tanzania amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kukubali kuwa mgeni
rasmi na kuongeza kuwa watahakikisha wanazingatia yote aliyoyasema Bw Magalula
na kunogeza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua maafisa uhamiaji wanaojihusisha na rushwa,
Mkuutano huo
wa siku mbili unashirikisha maafisa uhamiaji
wa mikoa sita ambayo ni Shinyanga,Rukwa,Kigoma,Kagera,Katavi na Simiyu lengo
kubwa likiwa ni kujadili jinsi ya kuendelea kupambana wahamijia haramu wanaorudi
nchini baada ya oparesheni kimbunga kuisha
Mkutano huu
ni wa pili kufanyika ndani ya mwaka huu na wa kwanza ulifanyika katika Mkoa wa
Rukwa na wa pili umefanyika mkoani Geita na unatajia kuisha hapo kesho.
Social Plugin