Baba mtarajiwa amezungumza kwa mara ya kwanza juu ya kuishi
bila kuwa na uso na kwa namna gani anahofia juu ya hali atakayozaliwa mtoto
wake mtarajiwa.
Anaitwa Mohammad Latif Khatana, 32, kutoka Kashmir, India,
hawezi kuona wala kufanya kazi kutokana na ngozi zilizofunika uso wake. Watu
humkimbia barabarani kutokana na hali yake huku wakionekana kuogopeshwa nayo.
Kwa sasa ni mwenye faraja kutokana na ukweli kwamba mke wake
ni mjamzito wa miezi saba, ila ana hofu labda huenda mtoto wake anaweza
kuzailiwa akiwa anfanana naye.
Alisema:
“Naingoja kwa hamu hii hali ya kuwa baba na kupata furaha ya maisha. Ila nahofu
kila siku na kusali ili mwanangu asije kuzaliwa kama mimi.”
Latif, ambaye
anaishi milimani na mke wake mwenye miaka 25 aitwaye Salima, eneo la Tuli Bana,
ndani ya Jammu and Kashmir, huwa anatembea mpaka Srinagar mara nne kwa mwaka
kwa ajili ya kuomba misaada na ili kupata hela.
Alizaliwa na
kinundu kidogo kwenye uso wake ila kimeendelea kukua na ktengeneza tabaka kubwa
la ngozi kwenye paji la uso wake, linalomfanya ashindwe kuona.
Anasema: “Mama yangu bado analia kila aniangaliapo, anajiona
kama mtu mwenye kosa na anashindwa kuelewa kwa
nini mtoto wake wa mwisho amekuwa hivi.”
Latif ni mdogo kati ya wakaka wawili na dada watatu huku
yeye pekee akiwa na tatizo hilo.
Bila ndugu zake angeweza kuishi maisha ya upweke sana udogoni kutokana na
kutokuwa na marafiki.
“Hakuna aliyetaka
kucheza na mimi utotoni,” akaongeza. “Wavulana kijijini kwangu walikuwa
wananipiga na kunitesa kila siku. Nilipoteza jicho langu la kushoto nilipokuwa
na miaka minane na wakawa wananiita mjinga mwenye jicho moja.”
Alipokuwa kijana
Latif alikumbana na changamoto mbalimbali za kimaisha. Ni mtu mwenye nguvu zake
ila kutokana na kushindwa kuwa anaona na kwa namna uso wake ulivyo hakuna
aliyeweza kumpa kazi.
Alisema:
“Ningependa kufanya kazi ya uhakika kama wanaume wengine wanavyofanya ili
kuweza kuzitunza familia zao, ingenifanya nijisikie fahari sana, ila hakuna
aliyenipa nafasi. Inabidi niombe na naamini watu wanaweza nisaidia ili
niweze kulisha familia yangu.”
Miaka minne iliyopita Latif alikutana na mwanamke wa maisha
yake, awali wazazi wake walijitahidi sana
kumtafutia mke ila hakuna msichana liyejitokeza, mpaka Latif aliposikia kuhusu
Salima.
“Mke wangu ana mguu mmoja tu na kwa muda mrefu amekuwa
akitafuta mume, punde tulipokutana tulijua tulikuwa sahihi kwa kila mmoja
wetu,” anakumbuka. “Wote tulikuwa hatujakamilika, hakika tuliendana.”
Walioana kwenye harusi ya Kiislamu wakiwa na wageni 400
mnamo August 2008 na wamekuwa wenye furaha toka kipindi hicho.
Akaongeza:
“Najiona nimebarikiwa sana kwa kukutana na Salima, ni mwanamke mzuri kwangu.
“Sasa naona
kawaida nina mke, ni kitu kikamilifu zaidi ya awali. Na sasa ana ujauzito wa
mtoto wetu wa kwanza nina furaha sana. Haijalishi kwa namna yoyote ile
nnavyoonekana ila sasa ni mwanaume mwenye furaha.”
Ila Latif, ambaye
hana maumivu na hapati matibabu yoyote, anahofu mtoto wake kama anaweza
kuzaliwa na hali kama aliyonayo yeye.
Anasema: “Hatuna
uwezo wa kumuona daktari, sisi ni masikini sana. Hakuna daktari kwa siku za
nyuma aliyenieleza nisipate mtoto. Ninakuwa na tumaini na kuomba kwamba mtoto
wetu atakuwa mwenye afya.”
Kaka yake na
Latif aliamua kuuza sehemu ya ardhi miaka minane iliyopita ili aweze kulipia
safari ya kwenda kumuona daktari ila hakukuwa na namna ambayo wangeweza
kuifanya.
Anakumbuka:
“Daktari aliniambia kwamba hali yangu ilitokana na mionzi ya jua wakati mama
alipokuwa na ujauzito wangu. Ila sijui kama nahitaji kumuamini.
“Na sasa kuna
vitu vingi vinanijia kichwani mwangu kwamba kufanya upasuaji inaweza kuwa ni
kitu cha hatari sana.
Nimepoteza
tumaini lote la msaada. “Hivi ndivyo nitakavyokuwa daima.”
Social Plugin