Bi Maria Charles aliyekutwa amejifungua katika mazingira machafu wiki iliyopita huko Kahama, akiwa amempakata mwanae wodini katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga |
Mtoto huyo wa kike ambaye bado hajapewa jina akiwa amelala katika wodi namba 5 katika hospitali hiyo |
Mwanamke mwenye matatizo ya akili ambaye alijifungua mtoto wa kike usiku wa kuamkia Jumamosi wiki iliyopita Bi. Maria Charles (32) kwa sasa anaishi vizuri na mtoto wake huku akiwa bado anapatiwa huduma katika hospitali ya wilaya ya Kahama katika wodi namba 5 alikolazwa mama huyo .
Kwa mujibu wa muuguzi mmoja aliyekutwa katika wodi hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema Bi. Charles anaonekana kumjali mtoto wake na pia kutii taratibu alizopewa hospitalini hapo kwani anatakiwa kila anapotaka kutoka nje akabidhi mtoto huyo kwa muuguzi wa zamu na amekuwa akifanya hivyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa muuguzi huyo mama huyo pindi atakaporuhusiwa kutoka hospitali atalazimika kumuacha mtoto huyo ili aweze kulelewa katika mazingira mazuri ya kiafya.
Siku ya Jumamosi wiki iliyopita Novemba 23 mwaka huu wasamaria walimkuta mama huyo akiwa amejifungua motto katika mazingiza machafu na bila msaada wowote na kisha kusaidia kumpeleka katika hospitali ya wilaya ya Kahama ili kupatiwa huduma za kiafya kwa mama na motto.
chanzo-Kiganjani blog
Social Plugin