Ni katika eneo lenye mgogoro,aliyesimama ni mwekezaji mzalendo aliyejulikana kama Paulo Majaliwa mkazi na mzawa wa wilaya ya Geita anayeendesha mradi wa kuchimba na kusaga mawe na kuuza kokoto |
Na Valence Robert-Geita.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
ccm mkoani Geita,Joseph Msukuma ametofautiana na serikali ya chama hicho
wilayani Geita,baada ya kuwarudisha kwa nguvu wananchi kwenye eneo la mwekezaji
lililopo katika kitongoji cha Nyantorotoro mjini Geita ambalo lina mgogoro wa
siku nyingi.
Mwenyekiti huyo alitoa amri hiyo
alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Nyantorotoro ambao baadhi yao ni waathirika wa mgogoro huo unaodaiwa
unatokana na baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa kuchochea
ili aondolewe mwekezaji huyo.
Msukuma aliwambia wananchi kuwa warudi kwenye maeneo hayo ambayo mwekezaji tayari ameishasimika mashine za kusaga mawe ili kupata kokoto kwa kutumia nguvu na ubabe.
“Nataka wananchi wote warudi kwenye maeneo yao ya mashamba na muendelee kuchimba mawe na hakuna mtu wa kuwagusa,awe mkuu wa wilaya,awe mkuu wa polisi au mkuu wa mkoa mimi ndo mwenyekiti wa ccm hakuna wa kuwagusa” alisikika huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo.
Eneo hilo
la Nyantorotoro ambalo mwenyekiti huyo aliagiza wananchi warudi kwenye maeneo
hayo linadaiwa kumilikiwa na mwekezaji mzalendo aliyejulikana kama
Paulo Majaliwa mkazi na mzawa wa wilaya ya Geita anayeendesha mradi wa kuchimba
na kusaga mawe na kuuza kokoto.
Alipoulizwa kuhusu uhalali wa
kimiliki eneo hilo
mwekezaji huyo,alisikitishwa na kitendo hicho cha mwenyekiti kulazimisha
wananchi kurudi katika eneo ambalo anafahamu kwamba linamilikiwa kihalali na
mwekezaji .
“ninamshangaa Musukuma kuongozana na viongozi
wa chama cha upinzani (CUF) na kuhamasisha wananchi kurudi kwenye maeneo
wanayojua ninayamilki kisheria tangu mwaka jana” alisema mwekezaji.
Aidha,alipoulizwa Afisa madini
mkazi wa Geita , Sementa Haruna kuhusu mmilki halali wa eneo
hilo la Nyantorotoro,alikiri eneo hilo kumilkiwa na Paulo Majaliwa kwamujibu wa
sheria ya madini kwa kufuata taratibu zote, “mmilki wa eneo hilo ni bwana Paulo
Majaliwa,ana leseni ambayo aliipata kihalali kwa mujibu wa sheria na ofisi yetu
ya madini inamtambua kwa namba ya leseni 000229LZ na 000238LZ
“Mimi nashangaa kwanini Msukuma haelewani na viongozi wenzake na wakati
wote wako chama kimoja na wapo kwa ajili ya kuongoza wananchi wa mkoa wa Geita
sasa wananchi wanashindwa waende wafate lipi.maana mwenyekiti anasema na serikali
inasema”,alisema Sementa.
Afisa ardhi wa wilaya ya Geita
,Venance Ngeleuya alisema “eneo hilo lilikuwa linamilikiwa na wananchi wa
Nyantorotoro Geita ikiwa bado mkoa wa Mwanza,TanRoads walipotaka kusaga
kokoto waliwahamisha wananchi hao na kuwalipo fidia wakaondoka,lakini wanasiasa
wamekuwa wanawalazisha wananchi kurudi kwenye maeneo hayo na kudai fidia
Aliendelea kusema kuwa wananchi hao
walilipwa na TanRoads lakini baada ya mwekezaji(Majaliwa )kumilki eneo hilo na
wananchi hao kushawishiwa na wanasiasa kudai fidia mara ya pili,mwekezaji
alikubali kuwalipa fidia na hadi sasa wanaomdai ni watu 8 kati ya watu 25
waliokuwa halali katika eneo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Geita Manzie
Mangochie alipoulizwa kuhusu uhalali wa mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi(ccm) mkoa wa Geita kutoa amri ya kurudisha wananchi katika eneo la
mwekezaji,alisema.
“ninashangaa mwenyekiti wa chama mamlaka ya
kutoa amri ya kurudisha wananchi hao ameitoa wapi na ametumia sheria ipi”
“ Ninachojua kuna taratibu za
kisheria zinazotakiwa kufuatwa lakini kwenye taratibu hizo mwenyekiti wa chama
hana nafasi ya kufanya hayo aliyo yafanya,yuko kinyume cha taratibu za
kisheria” alisema Mangochie.
,Mimi kama
mkuu wa wilaya naomba wananchi wafuate sheria wasidanganywe na wanasiasa
wanapotoshwa kabisa kwani sheria iko pale pale na zitafuatwa na kuzingatiwa.
Agizo hilo la mwenyekiti huyo
wa ccm mkoa wa Geita limekuja ikiwa ni zaidi ya mara tatu akitoa maagizo
yanayoashiria kuvunja sheria za nchi huku akiwaambia wananchi wanaweza kufanya
lolote ilimradi wameagizwa na kiongozi huyo wa ccm.
Baadhi ya maagizo aliyowahi kutoa
kwa wananchi katika mkoa wa Geita ni pamoja na kuwazuia wasifanye usafi katika
mji wa Geita kila Alhamis kama ilivyokuwa imeamriwa na kamati ya Afya ya
wilaya,kuzuia maafisa mistu wasikamate watu wanaokata miti na wachoma mkaa na
hivi karibu aliwaambia wananchi wa Bukombe kurudi kwenye pori walikokuwa
wamehamishwa na serikali.
Social Plugin