NB siyo Ng'ombe aliyeibiwa |
Wanakijiji wa kijiji cha Negezi tarafa ya Ukenyenge wilaya
ya Kishapu mkoani Shinyanga wamemuua kwa kumpiga mawe na marungu Majura Mayumba
(34) na kusababisha kifo chake papo hapo baada ya kuiba ng’ombe
Walioshuhudia tukio hilo wamesema kijana huyo ameuawa jana majira ya saa tatu usiku baada ya kuvamia nyumbani kwa Shija Kazara na kuiba
ng’ombe (maksai).
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku chache tu baada ya kijana mmoja mjini Shinyanga kuuawa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kuiba na kumchoma kisu mwendesha baiskeli,
Social Plugin