Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MZEE ANUSURIKA KUZIKWA AKIWA HAI AKITUHUMIWA KUUA KWA KUMLOGA BINTI MBEYA KIJIJINI

NB-hapa ni Iringa siyo Mbeya

Ikiwa  zimepita wiki takribani mbili baada ya mwanaume mmoja kuzikwa akiwa hai eneo la kijiji cha Mshewe wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, mwanaume mwingine wa kijiji cha Shilanga wilayani humo, amenusurika kuzikwa akiwa hai jana.
Taarifa kutoka eneo la tukio, zimemtaja mzee aliyenusurika kuzikwa akiwa hai kuwa ni Pascal Mwanjalanje, aliyetuhumiwa katika kifo cha binti mmoja kijijini hapo aliyekufa katika mazingira yanayodhaniwa kuwa ni ya utata.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shilanga, wamesema kuwa, kuna binti wa kijiji hicho alikwenda kufua mtoni na baada ya kumaliza aliwaambia wenzake kuwa anataka kupumzika, kisha akajilaza kwenye majani na kifo kikampata akiwa amejilaza.

Kutokana na tukio hilo, vijana wakachimba kaburi na kugomea kuuzika mwili wa mwanamke huyo kwa madai kuwa hakukuwa na mtu aliyekufa hivyo akatafutwa mzee Mwanjalanje anayetuhumiwa kumloga ili azikwe, na baada ya jitihada za kumzika mzee huyo kugonga mwamba walifukia kaburi.
chanzo-kalulungablog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com