Noma Kweli---!!! WANAOKAMATA WACHAWI MAARUFU KAMCHAPE NAO WAKAMATWA MKOANI TABORA
Friday, November 15, 2013
Baadhi ya Wataalamu wa kufichua watu wanaojihusisha na vitendo vya
ushirikina na uchawi maarufu KAMCHAPE wamejikuta wakiwa kwenye mikono ya dola
baada ya kuendesha zoezi la kufichua uchawi katika nyumba kadhaa kwenye
vijiji mbalimbali vya manispaa ya Tabora ambapo baadhi ya wananchi
walililalamikia zoezi hilo kwa madai kwamba limekuwa likiwadharirisha baadhi ya
watu pamoja na kujenga chuki ambazo huenda zikasababisha madhara makubwa katika
jamii. Wataalamu hao tayari wameanza kufikishwa kituo kikubwa cha Polisi mjini
Tabora kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya ambapo
aliwataka kuacha mara moja zoezi hilo
la kufichua wachawi
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin