Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia kijana mmoja kwa
tuhuma za kumbaka bibi kizee mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 na kumsababishia maumivu
makali katika sehemu zake za siri.
Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Singida Geofrey Kamwela amemtaja kijana huyo kuwa ni Saidi Hamisi (30) mkazi wa kijiji cha Wibia katika halmashauri ya wilaya ya Ikungi na kuongeza kuwa kijana huyo alitenda kosa hilo usiku wa kuamkia juzi majira ya saa sita.

Kamanda Kamwela amesema baada kufika kwa bibi huyo, kijana alivunja
fito za mlango wa nyumba hiyo ya kienyeji maarufu kama
tembe kisha kuingia ndani na kuanza kumbaka kikongwe huyo.
Hata hivyo amesema kutokana na kinachosadikiwa kuwa kunywa pombe za kienyeji kupita kiasi alikotoka, baada ya kumaliza kutenda unyama huyo mtuhumiwa alipitiwa na usingizi na kulala fofo.
Amesema hali hiyo ilitoa mwanya kwa bibi huyo kuamka taratibu kwenda chumba kingine walikolala wajukuu zake kuwaeleza mkasa uliomkuta, kisha kutoa taarifa kwa viongozi wa Kijiji na polisi.
Amesema mtuhumiwa alikamatwa na polisi masaa mawili baadaye ,baada ya kukutwa akiendelea kuchapa usingizi kitandani kwa bibi.
Kamanda Kamwela amesema mtuhumiwa anatarajiwa kupandishwa kizimbani wakati wowote kujibu shitaka la kuvunja nyumba na ubakaji mara baada ya upelelezi wa awali juu ya tukio hilo kukamilika.
Chanzo-Chamiwamatukio
Social Plugin