Ni muda mchache tu baada ya kukata utepe kuzindua jengo hilo askofu Malasusa anapanda mti nje ya kanisa hilo kubwa huku mamia ya waumini wa kanisa hilo na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo viongozi wa serikali mkoa wa Shinyanga na Simiyu wakishuhudia tukio hilo
Kushoto ni Askofu Malasusa kabla ya kuanza mahubiri akiwapungia mkono waumini waliohudhuria uzinduzi huo wa kanisa lenye sehemu mbili ambazo ni sehemu kwa ajili ya ibada lenye uwezo wa kukaa watu zaidi ya 1000 na sehemu ya pili ni ofisi kwa ajili ya kanisa hilo.Kulia ni Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria usharika wa
Ebenezer Kanisa Kuu Emmanuel Makala
Kwaya ya umoja ya kanisa hilo ikihubiri neon la mungu kwa njia ya uimbaji
Askofu Malasusa akihubiri wakati wa ibada ya ufunguzi na kuwekwa wakfu kwa kanisa hilo ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wanadamu kuwa wanyenyekevu mbele za bwana,kubeba msalaba na kumfuata bwana huku akisisitiza jamii kuachana na mauaji ya vikongwe kwa madai kuwa ni washirikina
Ibada inaendelea
Wa pili kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Annarose Nyamubi akifuatilia mahubiri ya askofu Malasusa
Kushoto ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam,pembeni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku wakiwa ndani ya kanisa hilo
Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria usharika wa
Ebenezer Kanisa Kuu Emmanuel Makala akizumgumza kanisani hapo ambapo aliwashukuru watu wote waliofanikisha kukamilika kwa ujenzi huo akiwemo waziri mkuu msaafu,ambaye sasa ni mbunge wa Monduli ambaye aliyechangisha harambee ya kwanza kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo ambapo hadi kukamilika limegharimu kiasi cha shilingi 1,231,659,590/= za kitanzania
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa jemgo hilo bwana Fredy Shoo akizungumza machache na kuwashukuru watu wote alioshirikiana nao hadi kukamilika kwa ujenzi huo
Profesa Mascky kutoka Japan ,rafiki yake na askofu Makala akizungumza kanisani hapo ambapo amewapongeza waumini wa kanisa hao ambao wameshiriki katika ujenzi wa kanisa hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Annarose Nyamubi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akitoa salaam za serikali ya mkoa wa shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine ameliomba kanisa kushirikiana na serikali katika kupiga vita mauaji ya vikongwe na albino
Social Plugin