Kuna
Sababu nyingi nana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano
yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Zifuatazo ni sababu 10 kati
ya sababu hizo;-
1. UONGO.
Hakuna
kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa
wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa
kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa
mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna
vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa
mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi
aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.
2. USIRI
WA KUPITILIZA.
Miongoni
mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora
kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa
moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya
moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta
ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama
kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora
umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana
kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya
kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa
mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi
ni kwa shingo upande.
3. ANA-CHEAT/ANA
MTU MWINGINE.
Hakuna
kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa
Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana
mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa
inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha
hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama
walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’
kwenye mapenzi.
Kamwe
Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye
Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji
Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo,
Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua
na si kwa ku-cheat.
4. DHARAU.
Hii
pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama
sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa
khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake
au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.
Na
hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi
mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata akili na mara nyingi sana
inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo, ila
wasichana wanatakiwa kutambua kuwa
6. TAMAA/KUKOSA
UVUMILIVU.
Tamaa
ni kitu kingine ambacho hufanya mahusiano mengi kukosa nguvu na mengine
kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye mapenzi na
mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na
kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.
7. KUKOSA
MSIMAMO.
Hii
kitu huwakuta wengi sana
kwenye mapenzi ya siku hizi. Nadhani ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia
pia pamoja na teknolojia tuliyonayo ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona
kwenye mitandao na vyombo mbali mbali vya habari.
Wapenzi
wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye mapenzi/mahusiano yao na unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi
zaidi ya mmoja na wanakuwa hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo
kila kitu kwa mpenzi wake.
8. KUTOJALI/KUTOKUWA
NA MSAADA.
Hii
pia kwa kiasi kikubwa inaumiza sana
na kupelekea kushuka kwa thamani ya mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi haa
duniani. Kama kweli unampenda mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo na
umjali na kumchukulia kama mpenzi wako na mtu
wako wa karibu na sio kukimbia majukumu bila sababu zote za msingi.
9. UBAHILI.
Huna
sababu yoyote ya kuwa na pesa na mpenzi wako akawa anapata tabu kama vile humuoni. Sijasema utoe pesa hata kwa mambo
yasiyo na msingi lakini at least utimize majukumu yako kwa mpenzi wako kila
unapohitajika.
Kuna
vitu vingine hata huhitaji kuambiwa kama
unatakiwa kuvishughulikia, ni wewe mwenyewe tu kuwa responsible kumhudumia
mpenzi wako. Na hii huwa ina-apply sana
kwa wavulana kutokana na kasumba iliyojengeka na mila tulizozikuta.
10. USHOGA/USAGAJI
Hii
ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu anayependa mtu wake awe Shoga kama ni
mvulana au awe Msagaji kama ni msichana. Ni aibu kubwa sana
kwa mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani kwa akili ya kawaida
kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama
utakishuhudia kwa macho yako.
Social Plugin