Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA HALI HALISI YA UKATILI DHIDI YA WANYAMA MKOANI SHINYANGA

Kamera za malunde1.blogspot.com  zimenasa tukio la wanyama aina ya punda wakiwa wamebebeshwa mzigo mzito wa mahindi kama unavyoona katika picha leo mjini Shinmyanga .Kubebeshwa mizigo mizito ni miongoni mwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanyama

sheria za kuzuia na kupambana na ukatili wa wanyama  zipo kama  vile sheria namba 154 ya mwaka 2010 ambayo
inasema kwamba mtu yeyote akifanya ukatili dhidi ya mifugo na ndege,mtu huyo anastahili kifungo cha mwezi mmoja au kulipa faini kiasi cha shilingi laki moja au vyote viwili
 

Lakini pia mbali na faini au kufungo hicho kwa wale wanaonyanyasa wanyama  ikiwemo kuning’iniza mifugo au ndege miguu juu kichwa pia  kuna faini ya papo kwa papo  ya  kiasi cha shilingi elfu hamsini.

Miongoni mwa  vitendo vya kikatili vinavyofanywa na binadamu dhidi ya wanyama hao kuwa ni kuwabebesha mizigo mizito, kuwafanyisha kazi kwa muda mrefu bila mapumziko, lakini pia kuwacharanga mapanga pindi wanapoingia kwenye mashamba ya watu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com