TAZAMA JINSI MAMBO YALIVYOKUWA KWENYE KILELE CHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SABA YA SIKU YA MLIPAKODI KATIKA MKOA WA SHINYANGA LEO
Friday, November 08, 2013
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Ally Nassoro Rufumga ,aliyekuwa mgeni rasmi akitoa hotuba katika kilele cha sherehe ya maadhimisho ya saba ya siku ya mlipakodi ,ambapo kimkoa zimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkoa wa Shinyanga.Mkuu wa Mkoa amesema serikali ya mkoa huo inaanza sasa kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara,ambao ni wadaiwa sugu wanaokwepa kulipa kodi.Lakini pia aliwataka watumishi wa mamlaka ya mapato mkoani shinyanga kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi huku akiwanyoshea mkono baadhi ya watumishi wanaotoa siri za wateja wao
Wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Mambo ndivyo yalivyokuwa hotuba ya mkuu wa mkoa inaendelea kuwagusa,miongoni mwa mambo aliyosema mkuu huyo wa mkoa ni kuitaka mamlaka ya mapato mkoa wa shinyanga kuwaburuza mahakamani biashara zenye matatizo,pia watumishi wa TRA kukusanya mapato kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuendelea kutoa elimu kwa walipa kodi juu ya umhimu wa kulipa kodi
Kwaya ya KKKT usharika wa shinyanga mjini ikitoa burudani na nyimbo zao nzuri zilizogusa mioyo ya watu waliohudhuria sherehe hizo moja ya nyimbo hizo ni ule unaosema"Tulipe kodi kwa matokeo makubwa,tulipe kodi kwa wakati unaofaa"
Meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga bwana Ernest Dundee akitoa hotuba yake leo ambapo alisema katika mwaka wa fedha uliopita yaani 2012/2013 mkoa wa shinyanga ulipangiwa kukusanya Tsh 14,115.0m kodi za ndani na wakafanikiwa kukusanya jumla ya Tsh 13,410.5 sawa na kiwango cha utendaji cha asilimia 95. na mwaka huu wamepangiwa kukusanya TSH 17,951.2m ikiwa ni ongezeko la Tsh 4,540.7 m.
Awali Mwenyekiti wa Chemba ya biashara ,kilimo na viwanda (TCCA)mkoa wa Shinyanga bwana Dickson Musula akizungumza leo
Mwakilishi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga,ambaye ni kaimu kamanda wa polisi mkoa ACP Kihenya Kihenya akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Ally Nasoro Rufunga,cheti ambacho jeshi limepewa ,ikiwa ni miongoni mwa taasisi/kundi la walipa kodi walioonesha mfano bora katika ulipaji kodi kwa mwaka 2012/2013
Mwakilishi klabu ya waandishi wa habari mkoa wa shinyanga Zuhura Waziri akipokea cheti cha walipa kodi walioonesha mfano bora mwaka 2012/2013
Bwana Isaack Edward Kisesa kutoka Radio Faraja akipokea cheti kwa niaba ya mkurugenzi wa radio kuwa nao ni miongoni mwa walipa kodi bora
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin