Shirika la viwango nchini TBS limepiga marufuku uuzaji wa
nguo za ndani za mitumba na atakayekamatwa akijihusisha na biashara hiyo hatua
kali zaitachukuliwa dhidi yao
Hatua hiyo imekuja baada ya kugundulika nguo hizo zinaleta madhara makubwa kwa watumiaji
Kufuatia tamko hilo shirika hilo tayari limeshaanza zoezi la kuingia katika masoko ya jijini Dar es Salaam kukamata wafanyabiashara hao
Afisa Uhusiano wa TBS, Rhoida Andusamile amesema wameamua kuingia katika masoko ili kuziondoa bidhaa kwani zinasababisha madhara kwa binadamu.
Amesema hatua hiyo imekuja kwa kuwa walitoa agizo miezi mitatu kabla kwa wafanyabiashara ili kuacha kuuza bidhaa hizo baada ya kubainika hazipo katika kiwango.
Amesema wameanza katika soko la Tandika na kufuatiwa na masoko mengine kwani bidhaa hizo hazitakiwi kuingia katika soko kwa mujibu wa sheria.
Zoezi hilo wamefanikiwa kuwakamata watu kadhaa huku wengine kukimbia
Social Plugin