WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATAKIWA KURUDISHA MAENEO YASIYOTUMIKA KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Na Valence Robert- Geita

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameiagiza wizara ya  nishati na madini kurudisha maeneo yote ambayo hayatumiki kwa wachimbaji wadogo

Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo  wakati akikagua shughuli za mchimbaji mdogo Bw Baraka Nyandu anayemiliki Mgodi wa dhahabu katika eneo la Nyaluyeye liliko wilayani Geita mkoa wa Geita.

Rais  Kikwete amesema kuna wachimbaji wakubwa wana maeneo lakini awayatumii hivyo kuitaka wizara inayaohusika kuwanyang’anya na kuwapatia wachimbaji wadogo na wazawa na watanzania.

Akikagua shughuli za maendeleo na kujionea shughuli zinazoendelea za uchimbaji na uchenjuaji kwenye Mgodi wa Ndugu Baraka Nyandu rais Kikwete amewataka watanzania kuiga mifano hiyo kuliko kukalia majungu yasiyo kuwa na faida kwao.

Mwekezaji huyo bwana Baraka Nyandu amesema kuwa Mgodi huo ulioa Mpaka sasa ametoa ajira kwa wazawa zaidi ya watu 350  na uendeshaji pamoja na kutoa misaada mbalimbali  na vyote vimegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 8 Milioni 70 na laki 9.

Mwekezaji huyo amesema pamoja na kufanikiwa  kuajiri watanzania wengi na kutoa misaada mbalimbali lakini bado  kuna changamoto mbalimbali zinazomkabili kama kukosa umeme na baadhi ya vifaa vya kuendeshea mgodi huo kupanda kwa kasi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post