NB -PICHA SIYO YA ENEO LA TUKIO |
Na Valence
Robert- Geita
Watu watano wamekufa
kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kutokana na kile kinachoelezwa kuiba rambirambi ya
shilingi elfu 65 katika familia ya mzee Luhemeleja aliyekuwa amefiwa na mjukuu wake.
Tukio
hilo limetokea leo mchana majira ya saa saba na nusu katika
kitongoji cha Nyantolotolo (A) nje kidogo ya mji wa Geita.
mashuhuda wa tukio hilo wamesema Mzee Luhemeja alifiwa na
mjukuu wake na baada ya msiba huo kuisha hapo jana watu wote wakiwepo
pia watuhumiwa wa tukio hilo walisambaa na kurudi
makwao.
Mashuhuda
wameongeza kuwa jana usiku watu wapatao wanane walifika nyunbani kwa mzee huyo kulikotokea msiba huo na kuingia ndani ambapo walimkuta mtoto mdogo na kumpiga
kofi baadae wakamfuata mzee wakampiga na kumuonba awapatie fedha kwa usalama
wake.
Baada ya kumpiga mzee huyo watuhumiwa walifanikiwa kuchukua
shilingi elfu 60 zinazodaiwa kuwa ni pesa za rambirambi zilizotolewa wakati wa
msiba baada ya mzee huyo kufiwa na mjukuu wake.
Imeelezwa kuwa baada ya kuchukua pesa kwa mzee
watuhumiwa hao na walimfuata mke wa mzee huyo ambaye jina lake halijafahamika
naye wakampiga na kumuumiza kisha kuchukua
kiasi cha shilingi elfu 5 toka kwake kisha wakatokomea kusikojulikana
Baada taarifa kusambaa kuwa kuna uvamizi
umetokea ,jeshi la jadi sungusungu lilianza msako na kufanikiwa kumkamata mmoja wa
watuhumiwa akiwa na damu kwenye nguo zake na kumhoji juu ya tukio hilo , mtuhumiwa akaanza kuwataja wenzake mmoja baada ya mwingine na jeshi hilo kuwatia mbaroni wote watano.
Baada ya watuhumiwa kutiwa mbaroni wananchi wenye hasira kali walianza
kuwashushia kipigo kisha kuwachoma moto hapo hapo huku mmoja kati ya hao watano akikatwa panga kwenye
mguu na kudumbukizwa kwenye kisima na kufia humo humo.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Geita
Dkt Adam Sijaona amekiri kupokea miili ya marehemu majira ya saa nane na nusu
mchana wa leo walioletwa na gari la polisi ambao walifika muda mfupi baada ya tukio wakiwa na
kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita
kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio na
kuwataja majina yao watu hao kuwa ni Juma Patrick Kigara,Marwa Chacha Kigara,na wawili
waliofahamika kwa Eze na Shija na wa tano akiwa hajafahamika jina lake.
Kamanda
Paulo amesema tayari watu watatu akiwemo kiongozi wa jeshi la jadi sungusungu wanashikiliwa
na polisi kwa mahojiano zaidi huku jeshi likiendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo .
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi wa habari hizi kutoka mkoani Geita
Valence Robert ni kwamba asilimia kubwa ya wanaumme wamekimbia miji yao
kutokana na msako mkali unaofanywa na jeshi la polisi kubaini wahusika wa tukio
hilo
Social Plugin