Ikiwa ni siku
chache baada ya gari la kubebea wagonjwa la kituo cha afya cha Nzera katika
halmashauri ya wilaya ya Geita kukamatwa mgodini likiwa na mapipa mawili ya
mafuta mali ya mgodi wa Geita Gold Mine,hali katika hali iliyoacha watu wengi
midomo wazi, hali hiyo imejirudia katika staili ya namna yake ambapo gari la ofisi ya uhamiaji mkoani Geita limekamatwa katika
mgodi huo wa [GGM] likiwa na dizeli pamoja na kiroba cha
mchanga.
Tukio hilo limetokea saa 2.30 baada ya walinzi wa mgodi kulitilia mashaka na kulazimika
kulisimamisha kwa ajili ya upekuzi na
kukuta mapipa ya dizeli na kiroba hicho ndani ya gari hilo lenye namba za
usajili T.690 AKW lililokuwa likiendeshwa na koplo Anorld.
Aidha baada ya gari hilo
kukamatwa gari hilo
lilipelekwa katika kituo cha polisi cha Geita na baada ya hapo likahamishiwa
ofisi ya uhamiaji.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa geita Bi Purudensia Poltas alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Gari hilo alisema hana taarifa zozote na kwamba
yeye hakuwepo alikuwa safarini
Naye afisa
habari wa Mgodi wa GGM bwana Tenga Bill Tenga amesema kuwa Gari hilo limekamatwa likiwa na kiroba cha mchanga Spana za
aina mbalimbali pamoja dizeli madumu madumu mawili ili vyote vikiwa ni mali za mgodi huo.
Afisa
uhamiaji wa mkoa wa Geita Bw Charles Washima alipotakiwa kujibu juu ya tuhuma
za gari hilo kukamatwa mgoini alisema kuwa gari hilo lilikuwa limepelekwa kwa
matengenezo na kwamba vifaa hivyo vilisahaulika ikiwa ni spana na lita saba za
oil tu.
Taarifa za gari hilo ni kuwa awali lilikuwa mali ya mgodi wa Geita Gold Mine
kabla ya kupewa ofisi ya uhamiaji mkoa wa Geita,na katika hali isiyokuwa ya kawaida
mwandishi wa habari hii bwana Valence Robert alipewa vitisho na kunusurika
kupigwa na mmoja wa watumishi wa ofisi ya uhamiaji mara baada ya kugundua kuwa
ameenda kuandika habari hiyo.
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin