Mkutano wa siku moja wa majaji wa nne (4) pamoja na mahakimu kutoka mkoa wa mwanza na Geita wa kujadili jinsi ya kuendesha kesi mbalimbali unatarajia kufanyika kesho tarehe 07/12/2013 mkoani Geita
Akiongea na vyombo vyambo vya habari ofisini kwake Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Geita Bw.DEUS KAMUGISHA ambaye atakuwa ni mwenyeji wa kutano huo amesema mkutano huo utaanza kesho saa tatu asubuhi na utafanyika katika Ukumbi wa Alfendo Hoteli ulioko mjini Geita
Ameongeza kuwa katika mkutano huo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa mkoa Geita Bwana Magarura Said Magarura katika mkutano huo pamoja na kujadili jinsi ya kuendesha kesi kutakuwepo na hoja mbili ambazo zitawasilishwa na majaji 2 ambazo ni UENDESHAJI WA KESI ZA MILATHI itakayowasilishwa na ANM SUMARI ambaye ni jaji mfawidhi mahakama kuu kanda ya mwanza ya pili UENDESHAJI WA KESI ZA NDOA NA TARAKA ambayo itawasilishwa na S.MWANGES Jaji mahakama kuu kanda ya mwanza ambazo zote zitajadiliwa katika mkutano huu
Bw.Kamugisha amesema japo majaji hao watawasilisha hoja hizo lakini watakuwepo majaji wengine wawili ambao ni Z.MERO Jaji mahakama kuu ya mwanza na Bw. Bukuku Jaji Mkuu Mahakama Kanda ya mwanza
Na mahakimu wa wilaya zote za mkoa wa mwanza lakini katika mkoa wa Geita zitashirikishwa wilaya 2 ambazo ni Geita Mjini na Nyagh’wale hizo ndiyo wilaya zitakazo shiriki katika mkutano huo.
Wanachama hao wa chama kinachojulikana kwa jina la JMAT
(Judges' and Magistrates' Association Tanzania )
ambapo mwenyekiti wake Bw.France Mwasiga ambaye ni mwenyekiti wa Tawi hilo atahudhulia mkutano huo
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin