Video ya Basi hilo tangU Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio majini na nchi kavu
Kampuni ya Transevents
Marketing Ltd ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious
Transport(DAT) linalotengeneza mabasi kutoka Uholanzi yenye uwezo
wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa
Afrika itakayoanzia Tanzania.
Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha
yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo
yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha sala zima la
usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo
wa kupita majini na Nchi kavu.
Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa
hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu. Mchakato huu umekwisha anza
kufanyiwa upembuzi yakinifu kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka
mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA ,
Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.
Credit-Michuzi
Social Plugin