Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangala |
Mzee Charles Abdallah Makune(87) mkazi wa kijiji cha Kahanga
kta ya Wendele wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga amemuua kwa kumpiga risasi
kichwani Mihangwa Maziku maarufu kwa jina la Mambe(40) mkazi wa kijiji hicho
kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni
mgogoro wa mashamba.
Kamanda wa jeshi la polisi
mkoani hapa Evarist Mangala tukio hilo amesema
tukio hilo limetokea
juzi majira ya saa moja asubuhi ambapo Mihangwa
Maziku akiwa nyumbani kwake alipigwa risasi kichwani na mzee Charles Abdallah Makune .
Amesema tukio hilo lilitokea baada ya kutokea hali ya kutoelewana kati yao katika mgogoro wa mashamba.
Kufuatia tukio hilo
wananchi walimshambulia kikongwe huyo kwa kumpiga na kitu kizito kichwani hali
iliyosababisha kikongwe huyo apelekwe katika hospitali ya wilaya ya Kahama
kupatiwa matibabu ingawa hata hivyo kikongwe huyo alifariki dunia wakati
akipatiwa matibabu
Social Plugin