Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo [SUA] umebaini kuwa
walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wapo katika hatari ya kupata ugongwa wa
kifafa kutokana na baadhi ya ngururuwe kuwa na minyoo inayopelekea ugonjwa huo.
Hayo yalibainishwa na Mhadhiri n a Mtafiti wa Idara ya Sanyansi ya
Wanyama na Uzalishaji SUA, Profesa Faustine Lekule alipokuwa akizungumza na
mwandishi kutoka chombo cha serikali.
Profesa
Lekule alisema, utafiti uliofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark
[DANIDA] ulibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa
ajili ya vipimo.
Uchunguzi
huo ulibaini kuwa, nyama hiyo kuwa na minyoo hatari iitwayo TEGU kuwa katika
nyama hiyo, hivyo endapo kama nyama hiyo
ikiliwa pasipo kuiva vizuri minyooo hiyo kawaida kukimbilia kichwani na hatima
yake mlaji kukumbwa na tatizo la kifafa.
Alisema
utafiti ulibaini baadhi ya wafugaji hawazingatiii kanuni za ufugaji na kuwaacha
wanyama hao kujitafutia chakula wenyewe na wanyama hao kupelekea kula hata
kinyesi cha binadamu, kutokana na wafugaji kujisaidia hovyo vichakani na ni
moja ya sababu ya wanyama hao kupelekea kupata minyoo hiyo.
Hivyo
binadamu nae anapokula nyama hiyo pasipo kuzingatia kanuni na kuila ikiwa
haijaiva vizuri hadi minyoo hiyo kuisha ndani ya nyama hiyo hupelekea kupata
madhara hayo kwa kuwa kuwa minyooo hiyo hukimbilia kichwani.
Alisema
ugonjwa huo hautaweza kukwepeleka kwa walaji wa nyama hiyo kwa kuwa nyama
nyingi husafirishwa na kusambazwa maeneo mengi na wanyama hao wengi hutokea
maeneo ya mikoani mikoa mikubwa yenye mapori.
Profesa
Lekule ameitaka serikali kwa ushirikiano wa wafugaji na wataalamu wa afya
kushirikiana kwa hali na mali kudhibiti ugon jwa na kukabiliana na changamoto
zilizopo kwakuwa,huo ambao ni hatari.
Credit-Nifahamishe
Social Plugin