Na Ali Lityawi- Kahama
Sababu ya wanawake kuongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) inatokana na kukosa maamuzi juu ya kutumia kinga
Hayo yalibainishwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga
jana na Mwezeshaji Kaskile Jumanne katika semina iliyoandaliwa na Shirika la
The Foundation for Human Health Society (HUHESO) inayotekeleza mradi wa
kuwakomboa wasichana wanaofanya biashara ya ngono, unaofadhiliwa na Rapid
Funding Envelop (RFE) ya jijini Dar es Salaam.
Jumanne ambaye ni Daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama,
alisema wanawake huathiriwa na mfumo dume wa kukosa maamuzi katika tendo la
ndoa jambo ambalo huchangia wakipata maambukizi kwa urahisi.
Alibainisha kuwa kwa jamii ambayo ni muumini mzuri wa kutumia
kondomu lakini baadhi ya watu pia hujikuta wakipata maambukizi mapya kutokana
na kutofahamu matumizi sahihi wakati wa kuvaa, kuivua na kuhifadhi baada ya
matumizi.
Mkurugenzi wa HUHESO, Juma Mwesigwa alisema wanawake wanapaswa
kubadilika na kuondokana na jukumu la mapenzi kutawaliwa na mwanaume ili
kuondokana na hatari ya kupata maambukizi mapya.
Mwesigwa alisema wanawake hawana budi kujitambua kwa kubadilika
na kuwa jasiri jambo litakalosaidia kupunguza maambukizi.
|
Social Plugin