Marehemu anayedaiwa kuanguka na ungo kisha kuuawa na wananchi |
Wananchi wakisulubu kijana huyo |
Wananchi waliojichukulia sheria mkononi, wenye hasira kali
wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya
kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo mkazi wa
Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa
12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za
kishirikina.
Kabla ya kufariki
alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita,
wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa
tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”
“Lakini mimi kwa bahati
mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla
nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”
Hata hivyo kutokana na
vurugu zilizokuwapo eneo hilo la
tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa
wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na
kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa
tukio hilo walisema
baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa
pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na
ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.
“Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa,
sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko
alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana
zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi
walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo
Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa
taarifa
mapema.
“Sisi tumepiga simu kituoni hapo
hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa
12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa
eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali.
Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi
mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo
la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani
waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.
Waandishi wa habari hodi katika
kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho
zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa
maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho
ndiyo wenye dhamana.
Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M.
Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa
kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha
tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokelewa.
Credit Mtanzania
Social Plugin