Mahakimu na majaji wa mikoa ya Mwanza na Geita
wameaswa kuendelea kuhukumu kesi za wananchi wa mikoa hiyo bila kujali masikini
au tajiri,na kuacha kulundika mafaili ya watuhumiwa,kama ilivyo hivi sasa.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa
Geita Bwana Magarura
Said Magarura kwenye mkutano wa chama cha majaji [4] pamoja na
mahakimu zaidi ya sabini kinachojulikana kwa jina la[JMAT] waliotoka
mikoa ya Mwanza na Geita ambao umefanyika jana Jumamosi katika ukumbi wa Alifendo Hotel ulioko mjini
Geita.
Mkutano huo uliokuwa na lengo la
kutatua migogoro ya ndoa pamoja na mirathi.
Magarura amesema japokuwa
kuna mahakimu wanawatendea haki wananchi lakini kuna baadhi ya mahakimu
wanafanya kazi kwa kuangalia uwezo wa mtu kama ni tajiri au masikini hivyo kama
wapo wanaowanyima haki wananchi basi waache tabia hiyo mara na wasipoacha
watachukuliwa hatua kali kwani kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu
kutotendewa haki kwenye kesi zao na mahakimu.
Magarura ameongeza kuwa majaji hao pamoja na mahakimu wanatakiwa
kutumia mkutano huo kujifunza na kuachana na mapungufu wanayokabiliana nayo
ikiwa ni pamoja na kuendelea kuhukumu kesi za wananchi kwa haki.
Naye A.N,M Sumari ambaye ni jaji mfawidhi
Mahakama ya kanda ya Mwanza alimshukuru mkuu wa mkoa wa Geita kwa
kukubali kuwa mgeni rasmi na kuahidi kuyafanyia kazi yote yaliyosemwa na mkuu huyo
na kuahidi kuwachukulia hatua kali baadhi ya mahakimu wanaojihusisha na Rushwa
kwenye mahakama mbalimbali za kanda ya Mwanza.
Bi Sumari ameongeza kuwa pamoja na
hayo kumekuwa na changamoto mbali mbali zizowakabili ikiwa ni pamoja na kukoa
ofisi na vitendea kazi vichache kwenye
mahakama mbali mbali za kanda ya Mwanza na Geita na kumuomba kuwasaidia pale
wanapokuwa na shida.
Na Valence Robert -Geita
Social Plugin