Majambazi watatu wameuawa wakati wakirushiana risasi na polisi wakati majambazi hayo yakiwa katika harakati za kuvamia mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema tukio hilo limetokea majira ya saa sita usiku katika kijiji Namba Tisa,kata ya Bulyanhulu ambapo watu
hao wasiofahamika jina wala makazi yao
umri kati ya 25-30 walikuwa wanajiandaa kuvamia mgodi
Kamanda Mangala amesema majambazi hayo yalikuwa na mabomu
matatu ya kurusha kwa mikono, bunduki aina ya SMG mbili na risasi 94.
Social Plugin