Picha ya jambazi lililouawa kwa risasi baada ya kuvamia hivi karibuni huko Kahama |
Watu
watano wanaodaiwa kuwa ni majambazi wnashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga muda mchache tu baada ya kuvamia duka la mfanyabiashara mmoja na
baadaye kuvamia nyumba ya mfanyabiashara mwingine katika kijiji hicho.
Tukio hilo limetokea juzi majira
ya saa mbili usiku ambapo majambazi hao walimvamia Mussa Bernard Bugani(38)
mfanyabiashara na mkazi wa kijiji hicho akiwa dukani kwake na kupora pesa,vocha
za simu.
Kaimu kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya amesema baada mkali uliendeshwa na
wananchi kwa kushirikiana na waya tukio hilo jeshi la polisi na wananchi wa
kijiji cha Lunguya na kufanikiwa kukamata majambazi hao pamoja na bunduki moja
aina ya SMG yenye namba za usajili UA-42571997 na risasi 26.
Kamanda
Kihenya amewataja majambazi hao kuwa ni Bakari Ramadhani Lumala(31),mfanyabiashara,AmonLubisi(24),mfanyabiashara,Emmanuel
Petro Charles(20) wakala wa Airtel Money,Pius Ernest Samson(34) mkulima pamoja
na Silas Iselubisi(25) mkulima wote wakazi wa Segese wilayani Kahama.
Social Plugin