Mwanamme
mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ameuawa kikatili kwa
kupigwa mawe na fimbo kisha mwili wake kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa kuiba
ng’ombe wawili kwenye zizi la mkazi wa kijiji hicho wenye thamani ya shilingi
laki 8 katika kijiji cha Mwanima kata ya Sekebugoro wilaya ya Kishapu mkoani
Shinyanga.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Kihenya Kihenya alisema tukio hilo limetokea jana saa tisa na
nusu mchana baada ya mwanamme huyo ambaye hakuweza kufahamika jina kabila wala
makazi yake baada ya kudaiwa kuiba ng’ombe,wananchi walijichukulia sheria
mkononi kwa kumshambulia kwa kumpiga fimbo na mawe kisha kumchoma
moto na kusababisha kifo chake.
Ni siku chache tu zimepita
ambapo mwanamme mwingine aliyefahamika
kwa jina la Majura Mayumba (34) mkazi wa kijiji cha Negezi tarafa ya Ukenyenge
wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga aliuawa kwa silaha za jadi baada ya kuiba
ng’ombe mmoja mwenye thamani ya
shilingi laki 5 katika kijiji hicho.
Social Plugin