Mwanamke mmoja aitwaye Kwezi Seleli (20) ameuawa kwa kuchinjwa na mme
wake wakiwa wamelala nyumbani kwa katika kijiji cha Kalama,kata ya Uyogo
wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo
limetokea jana saa kumi alfajiri Chalia Samweli (25) mkazi wa kijiji hicho,alimchinja
mke wake kwa kutumia panga na baada ya mauaji jamaa akafanya jaribio la kujiua
kwa kunywa sumu aina ya Diazone
inayotumika kuogeshea mifugo bila mafanikio.
Jeshi la polisi mkoa
wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kwamba uchunguzi kuhusu tukio hilo
unafanyika.
Social Plugin