Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mauaji!!! JAMBAZI LAUAWA WAKATI LIKIVUNJA NYUMBA HUKO KAHAMA,TAZAMA HAPA PICHA NA STORI

Mzee Masolwa aliyeua jambazi

Mwili wa jambazi hilo ukiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama
Mwanamme mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja jina,kabila wala makazi yake (26-30 ambaye ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa katika harakati za kuvunja nyumba katika mtaa wa Shunu,kata ya Nyahanga wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa nane na nusu ambapo jambazi hilo likiwa na wenzake watatu liliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na mkazi wa mtaa huo wa Shunu  bwana Wilson Masolwa (65) anayeishi jirani na nyumba ya
Yasinta Patrick (32) mkazi wa mtaa huo,ambaye ni mfanya biashara mjini Kahama .

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema huenda lengo la majambazi hao lilikuwa ni kuiba pesa katika maduka ya M-PESA yaliyopo katika nyumba ya Yasinta kwani baada kufika eneo hilo walifunga kwa nje maduka mawili wakijua kuwa ni ya Yasinta kisha wakamfuata Yasinta katika chumba kingine alichokuwa amelala na kumtaka atoe pesa .

Majeruhi katika tukio hilo bwana Wilson Masolwa amesema baada  kusikia kelele kutoka kwa jirani yake alifika katika eneo la tukio majambazi hao walianza kumcharanga mapanga sehemu za mkononi na sehemu zingine za mwili ndipo aliamua kumtwanga risasi kichwani mmoja wa majambazi hao

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya  na kwamba kufuatia majeraha aliyopata Wilson Masolwa alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya matibabu na kwamba hali yake inaendelea vizuri huku akitaja chanzo cha tukio hilo kuwa ni kuwania mali na kwamba jeshi la polisi linaendelea na msako mkali wa kuwabaini na kuwakamata wahusika pamoja na bunduki iliyoporwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com