Mwili wa marehemu bibi Lucia aliyeuawa kikatili kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina
Marehemu akiwa katika eneo alilokuwa akila chakula na wajukuu zake |
Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Lucia Mgonga (55) mkazi
wa kijiji cha Mega wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kukatwa Mapanga
na watu wasiojulikana.
Tukio hilo
la kutisha limetokea Usiku wa kuamkia juzi majira ya saa mbili usiku wakati
bibi huyo akiwa na wajukuu zake wakipata chakula cha jioni.
Marehemu amepoteza maisha baada ya kukatwa
panga sehemu ya bega lake la kushoto na Shingoni.
Imeelezwa kuwa sababu ya mauaji hayo kuwa ni
imani za kishirikina.
chanzo-Dunia Kiganjani blog
Social Plugin