Ukol Talumpa enzi za uhai wake |
Sasa hivi matukio ya watu kupigwa risasi kwenye mikasa ambayo sio ya kawaida sio Tanzania tu bali hata kwenye nchi nyingine au maeneo mengine ambayo hayakuwahi kuwa na rekodi za ukatili wa aina hii. Taarifa ya leo inamuhusu Meya wa mji wa Labangan nchini Philippine ambaye amepigwa risasi akiwa na watu wengine watatu maeneo ya airport huko Manila Philippine ambapo Ukol Talumpa imeripotiwa alipigwa risasi pamoja na mke wake, mtoto wao wa miezi 18 na mtu mwingine mmoja na kufariki dunia. Ripoti hii inasema watu wengine wanne wamejeruhiwa kwenye tukio hilo wakati mshambuliaji huyo alipotekeleza shambulio hilo huku kiongozi huyo aliekuwa nje ya terminal 3 ya Airport akisubiri usafiri ambapo ndio mtu mmoja akiwa kwenye pikipiki alipita na kufyetua risasi kwa karibu na kukimbia na pikipiki yake. Chanzo cha tukio hili bado hakijajulikana. |
Social Plugin