NB PICHA KUTOKA MAKTABA YA MALUNDE |
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) (NEC)
Khamis Mgeja ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga amewashauri baadhi ya mawaziri hapa
nchini kuacha tabia ya kuzinyanyapaa ofisi za chama cha mapinduzi CCM pindi
wanapokuwa katika ziara za kikazi katika wilaya na mikoa kwani katika ofisi
hizo ndipo kwenye taarifa mbalimbali za
kero za wananchi.
Akiwahutubia
wanachama na wananchi wakati wa ziara yake mkoani shinyanga mwishoni mwa wiki iliyopita amabpo Mgeja alisema baadhi ya mawaziri wanaofanya ziara
za kikazi mikoani na wilayani wamekuwa na
tabia ya kukimbilia katika ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya na hata
pale wanapokwenda katika ofisi za CCM huchungulia mara moja na kuondoka baada
ya kuweka saini katika vitabu vya wageni badala ya kufika katika ofisi za chama
na kusikiliza kero za wananchi.
Mgeja alisema endapo mawaziri watajenga utamaduni wa kufika katika ofisi za
chama wataelezwa kero hizo, watapewa ushauri jinsi gani wazipatie utatuzi,na
ushauri wa nini kifanyike katika kuboresha zaidi utendaji ndani ya wizara zao,
lakini pia wataelezwa ni watendaji gani wa serikali katika wilaya ama mkoa
wasiotimiza wajibu wao.
Mjumbe huyo wa NEC
alisema ni vizuri mawaziri hao hivi sasa wakabadilika na waache kufanya kazi
zao kwa mazoea hali ambayo itasababisha chama kihukumiwe kwa makosa ambayo siyo
ya kwake, na lazima waelewe CCM hivi sasa imechoka kubeba mizigo ya lawama
zinazotokana na uzembe wa baadhi ya mawaziri ndani ya serikali.
Social Plugin