MWANDISHI WA RADIO FREE AFRICA ASHAMBULIWA NA KUNDI LA ASKARI POLISI WA GEITA,APASULIWA MISHIPA YA JICHO

Na Valence Robert-Geita
Mwandishi wa Habari wa Redio Free Afrika Mkoani Geita Bw Salum Maige amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita  mkoani Geita baada ya kujeruhiwa vibaya sana kutokana na kushambuliwa na kundi la Askari polisi wa kituo cha polisi Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari  Bw maige ambaye amelazwa katika chumba NO,4 wodi No 2 katika hospitali ya wilaya hiyo amesema alishambuliwa jana majira ya saa moja kamili usiku na kundi la askari polisi zaidi ya watano akiwa umbali wa mita 60 kutoka zilipo ofisi za polisi mkoa pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa,

Amesema siku hiyo akiwa anatoka eneo hilo akielekea nyumbani kwake mtaa wa Bomani alikutana na kundi hilo la polisI waliokuwa na gari NO,za usajili PT 1998 ocd Geita ambapo baadhi yao walishuka kutoka kwenye gari na kumueleza kwaMba yuko chini ya ulinzi anaitajika polisi mara moja,

Ameongeza kuwa alilazimika kuwauliza polisi kosa lililosababisha ahitajike polisi lakini badala ya kumjibu walimshika na kufunga pingu mikononi kisha kumtupia ndani ya gari na kumshambulia kwa kipigo na huku akiwa amekanyagwa kichwani.na askari awo.

Kufuatia kipigo hicho Maige  amejeruhiwa vibaya jicho la upande wa kushoto ambapo kwa mujibu wa Daktari aliyemfanyia uchunguzi kwenye jicho amesema amepasuka mishipa yake  kwa ndani kutokana na kipigo  hicho hali iliyosababisha damu nyingi kuvuvjia ndani ya jicho,

“Kwakweli amepasuka mishipa na hatujui kama itapona lakini tunajitaidi kumpa huduma lakini nawashangaa awa polisi hawana hata huruma huyu wanamfahamu wamemfanyia hivi je kama hawakujui si wanakuua kabisa” alisema dakrai huyo.

Akifafanua zaidi  kuhusiana na tukio hilo Maige  amesema katika siku za hivi karibuni amekuwa katika mgogoro wa kifamilia na mkewe hali iliyosasababisha mkewe kwenda kumshitaki polisi ambapo polisi waliamua kwenda kumkamata kabla hata ya kufungua mashitaka na baada ya kufikishwa polisi ndipo alipokuta mkewe na kuanza kumfungulia mashitaka,

Hata hivyo katka hali ya kushangaza pamoja  na kujeruhiwa vibaya polisi walikataa kumpatia fomu kwa ajili ya kwenda kupata matibabu hali iliyosababisha kushindwa kupata matibabu hadi leo asubuhi ambapo baadhi ya waandishi walilazimika kwenda naye polisi na kudai apatiwe fomu hiyo na kwenda kupatiwa matibabu.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Leonard Paul hakupatikana kuzumgumzia tukio hilo la shambulio dhidi ya mwanahabari huyo lakini kaimu wake Bi Pudensiana Protas alithibitisha kupewa taarifa juu ya kukamatwa kwa mwndishi huyo lakini hakujulishwa juu ya kupigwa kwake.

Hata hivyo baada ya kuoneshwa picha za majeraha ya mwandishi huyo ofisini kwake alionekana kushutuka na kuahidi kwenda hosptalini kufanya mazungumzo na mwandishi huyo na kwamba baada ya hapo atafuatilia suala hilo kabla ya kulitolea maelezo ya kina.

Tukio hilo limewaachia na maswali mengi baadhi ya wananchi na waandishi wa habari wa mkoa wa Geita wanaojiuliza  je kwa tuhuma za madai yaliyowasilishwa juu ya mgogolo wa kifamilia kati ya mwandishi huyo na mkewe ilikuwa sababu ya yeye kutafutwa na askari zaidi ya 5 tena wakiwa na bunduki gari na kumkamata na kumtia pingu kisha kushambulia kwa kipigo  kama jambazi ama kuna jambo jingine nyuma ya pazia.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post