Neema yaiangukia Kishapu!!! MRADI WA KUIJENGEA JAMII UWEZO WA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA KWA MIKOA ILIYOATHIRIKA ZAIDI NA UKAME WAZINDULIWA,KISHAPU NI WILAYA PEKEE MKOA WA SHINYANGA KUNUFAIKA


 Mkurugenzi wa idara ya uratibu wa maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu,luteni jenerali Sylivester  Rioba mapema leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuijengea jamii uwezo wa kupunguza athari za maafa kwa mikoa  iliyoathirika zaidi na ukame kama vile mkoa wa Kilimanjaro na Shinyanga,uzinduzi ambao umefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu na Kishapu ndiyo wilaya pekee katika mkoa wa Shinyanga ambayo itanufaika na mradi huo unaofadhiliwa na benki ya dunia
Katibu tawala wa wilaya ya Kishapu  bwana Octavian Mangosongo akizindua mradi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambapo pamoja na mambo mengine utahusisha kuelimisha vijana na akina mama juu ya upndaji miti na kilimo cha mazao yanayohili ukame hususani mihogo  na viazi vitamu pamoja na kuaninisha na kutoa mafunzo kwa wadau kuhusu matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo,mifugo na misitu lakini pia upatikanaji wa maji safi na salama.

Aliyesimama ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu bwana Justin Sheka akizungumza wakati wa uzinduzi ho wa mradi wa kuwawezesha wananchi katika kupunguza athari za maafa na katika wilaya ya Kishapu miradi ya ,majaribio itaanzia itafanyika katika kata ya Masanga  na Mwamalasa .Sheka amesema kama mradi huo utatekelezwa ipasavyo utakuwa mkombozi wa maisha ya wakazi wa Shinyanga

Wadau mbalimbali waliokuwepo wakati wa uzinduzi huo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu
Wadau muda mchache baada ya uzinduzi wa mradi huo ambao unategemewa kuwa suluhisho la maafa mbalimbali katika wilaya hiyo kama vile ukame unaopelekea kuwepo kwa upungufu wa chakula wa mara kwa mara 

Baada ya uzinduzi huo,Picha ya pamoja kwa wadau waliohudhuria uzinduzi  wakiwemo wakina mama,vijana,walimu wakuu,idara na asasi mbalimbali,wilaya na  mkoa kwa ujumla,waandishi wa habari na wengine wengi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post