Ni Balaa!!! TAZAMA HAPA YALIYOJIRI UWANJA WA SHY-COM WAKATI WA BONANZA YA DIWANI WA MJINI SHINYANGA ,MHESHIMIWA GULAM HAFEEZ ABUBAKAR MUKADAM,AMBAYE PIA NI MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA
Thursday, December 12, 2013
Mapema leo diwani wa kata ya mjini shinyanga (aliyeko mbele) Mheshimiwa Gulamhafeez Abubakar Mukadam,ambaye pia ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga akiongea na wachezaji mpira wa netiboli timu ya mtaa Buzuka (jezi nyeupe) na timu ya Kaunda kabla ya kuanza kufanyika kwa mechi ya fainali kati ya timu hizo ambapo aliwapongeza kwa kuendelea wavumilivu katika siku zote za mashindano hayo ya Diwani cup kata ya mjini Shinyanga pamoja na kwamba mvua imekuwa ikinyesha kila siku jioni
Mechi kati ya Kaunda na Buzuka wakicheza leo wakati wa Bonanza lilioandaliwa na Diwani wa kata ya Mjini Shinyanga ambapo Buzuka walipata seti 11 huku Kaunda wakipata seti 15 hadi mwisho wa mchezo na kufanikiwa kunyakua kombe na pesa taslimu shilingi elfu 75,na wenzao kuambulia shilingi elfu 75.
Mheshimiwa diwani wa kata ya mjini Shinyanga Gulam hafeez Mukadam kupitia Chama cha mapinduzi CCM akishikana mkono na wachezaji timu ya mtaa wa Miti mirefu na Buzuka fc waliofikia hatua ya fainali
Mechi kati ya Miti mirefu fc (jezi kijani) wakipambana na timu ya Buzuka fc leo katika uwanja wa Shy-com mjini Shinyanga
Ni katika jukwaa kuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika uwanja wa shycom wakati wa Bonanza iliyondaliwa na diwani wa kata ya mjini shinyanga mheshimiwa Mukadam ambaye ambaye alikuwa ameugua kwa muda mrefu na kwenda kutibiwa nchini India na sasa hali yake inaendelea vizuri na kuanza kuchapa kazi katika kata yake kwa nguvu zote
Wakazi wa Shinyanga wakishuhudia kilichokuwa kinajiri uwanjani hapo katika bonanza ambayo imeshirikisha mitaa mitatu ya kata ya mjini shinyanga yaani mtaa wa Kaunda,Buzuka na Miti mirefu
Mambo yalikuwa mazuri kiasi cha kuwafanya hadi waendesha baiskeli maarufu daladala ambao hubeba abiria kutoka sehemu moja hadi nyingine wakaamua kusitisha kazi zao na kuangalia michezo iliyokuwa inaendelea mfano mpira wa miguu,netiboli,kukimbiza kuku,kuvuta kamba,riadha na kukimbia kwenye magunia
Mchezo wa kuvuta kamba nao ulikuwepo kama unavyoona hapo juu.Bonanza imesimamiwa na viongozi wa mitaa ya Kaunda,Buzuka na Miti mirefu
Washiriki wa mchezo wa kuvuta kamba kutoka mtaa wa Kaunda wakiwa wamezidiwa nguvu na kujikuta wakianguka
Ilikuwa ni burudani sana,bonanza iliyofadhiliwa na diwani wa kata hiyo na kupata ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa viongozi wa mitaa ya Kaunda,Buzuka na Miti mirefu
Mchezo wa kukimbiza kuku nao ulikuwepo ,wazee kutoka mitaa hiyo wakikimbiza jogoo uwanjani hapo
Mbio za magunia nazo zilikuwepo
Mheshimiwa diwani wa kata ya Mjini Shinyanga,ambaye pia ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Mukadam akikabidhi pesa kiasi cha shilingi laki moja kombe kwa washindi upande wa mpira wa miguu,ambapo Buzuka Fc waliibuka washindi na kupewa kombe huku washiriki wengine wakipata shilingi laki moja kila mmoja
Kila mshiriki alipata zawadi, hapa Washindi katika riadha mita 100 wakiwa wameshilia zawadi zao
Mashindano hayo yaliyodumu kwa muda wa siku yakishirikisha mitaa mitatu mwandaaji wake,Diwani wa kata hiyo Mukadam alisema lengo ni burudani ,,kuendeleza michezo katika kata hiyo na kuleta mshikamano kwa wakazi wa kata anayoiongoza baada ya kusimama kwa muda baada ya yeye kuugua,ambapo pamoja na kufanyika kwa Mashindano hayo maarufu kwa jina la Diwani cup,ambayo yamehitimishwa kwa bonanza ,yatafuatiwa na mashindano katika shule za kata hiyo baadaye ngazi ya manispaa ya shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin