Katana Kitsao anayedaiwa kumla uroda mbuzi |
Mbuzi anayedaiwa kubakwa
Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 28 amehukumiwa kwenda jela
miaka kumi mara baada ya kukutwa na hatia ya kufanya tendo la ngono na mbuzi.
Katana Kitsao Gona toka Malindi nchini Kenya wiki iliyopita alikiri
kufanya ngono na mnyama.
Mbuzi huyo wa kike kwa utulivu alikuwa
pembeni ya chumba cha mahakama wakati hukumu hiyo ilipokuwa inatolewa. Jamaa
huyo alikamwatwa mnamo tarehe 25 Novemba mara baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo kumbamba akiwa uchi wa
mnyama akimla uroda mbuzi huyo ambaye alikuwa amefungwa kamba, hii ni kwa
mujibu wa The Star.
Mmiliki
wa mbuzi huyo alifahamishwa na kufika eneo la tukio akiwa na majirani wengine
ambao pia walimshuhudia Gona akiwa anafanya ngono na mnyama.
Jamaa alikamatwa na polisi na vipimo vya hospitali
vinakaonyesha kweli kwamba tukio la ngono lilifanyika.
Gona aliomba msamaha kwa
mahakama kwa kujitetea kuwa mke wake ni mlemavu na anamtegemea yeye ila
mahakama ikajibu kuwa kosa hilo
ni kubwa na akapewa siku 14 za kukata rufaa.
Social Plugin