Kingwendu |
Mr Bondi aliskika hivi karibuni akizungumza kwa njia
ya simu katika Radio moja hapa jijini Dar esa Salaam akimlaumu Vikali Msanii
Mwenzake
Kingwendu kumtapeli shilingi Laki 2 alizompa kama advance ya Kufanya
shooting ya Move yao Mpya ambayo Wamo Mastaa kibao akiwemo Yeye Mr
Bondi,Natasha,Monalisa na Wengine Kibao.
Alichokifanya
Kingwendu ni kutoonekana siku ya kufanya hiyo filamu na kuzima simu zake kwa
siku sita bila taarifa yeyote na mbaya zaidi alimdanganya Mr Bondi kuwa mama
yake anaumwa hivyo anaenda kumwona ila atawahi kurudi kabla ya siku ya
shooting.
Taarifa zaidi
ni kwamba Kingwendu alipata show nchini Msumbiji.Baada kutafutwa na waandishi
wa habari Kingwendu alisema ni kweli Mr
Bondi alimpa laki 2 kama advance na alikuwa Tayari kufanya hiyo kazi ila kwa
Bahati nzuri alipata show Msumbiji na waliompa show walimdanganya kuwa
wamemkatia tiketi ya ndege ya go and return hivyo alijua angewahi.
Kingwengu
alisema mbaya zaidi alipofika kule ikawa shida kurudi baada ya kukosa
ndege.Hivyo ilibidi asubiri Ndege.
Hata hivyo
amemuomba radhi Mr Bondi kwa kitendo alichokifanya na Anamuomba amsamehe sana yeye ni Binadamu na
kilichomponza ni Ndege,alijua angewahi.
Chanzo-babamzazi
Social Plugin