Mtoto mmoja
aliyefahamika kwa jina la Jirungu
Gerald (4)mkazi wa Kijiji cha Mwandulu kata ya Lagana tarafa ya Negezi wilayani
kishapu Mkoani Shinyanga amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na pikipiki .
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Shinyanga ACP Kihenya kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio ambalo
limetokea jana majira ya saa kumi na mbili jioni baada ya mwendesha pikipiki
kumgonga mtoto huyo na kusababisha kifo chake baada ya kushindwa
kumkwepa mtoto huyo.
Amemtaja mwendesha pikipiki huyo kwa
ni Paulo Martine mkazi wa
kijiji cha Sanjo wilayani humo aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za
usajiri T,464 CPD aina ya T,BETTER mali ya Felis mfanyabiashara wa mjini Shinyanga
Ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni
mwendo kasi na kuongeza kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la polisi huku
akitoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama
barabarani pamoja na wazazi kuchunga watoto wenye umri mdogo wasicheze
kandokando ya barabara
Social Plugin