Mwanamme mmoja aitwaye Godi Shaini Fanuel Mangala (34) mkazi wa mtaa wa Majengo Mapya kata ya Ngokolo mjini Shinyanga amefariki dunia kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni kunywa pombe aina ya konyagi kupita kiasi.
Mashuhuda wa tukio hilo wameimbia malunde blog kuwa tukio hilo la kusikitisha limetokea siku ya krismasi Desemba 25 mwaka huu saa moja jioni.
Wamesema marehemu alikuwa anakunywa pombe na wenzake katika moja ya Glosary mjini Shinyanga na baadaye mwenzao alizidiwa na kulazimika kurudishwa nyumbani kwake ili akapumzike na hali ilipozidi kuwa mbaya wakampeleka katika hospitali ya mkoa lakini akafariki dunia akiwa njiani
Hata hivyo mmoja wa mashuhuda hao ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa anashindana na wenzake kunywa pombe maarufu konyagi ama wengine wanapenda kuziita Bapa.
Diwani wa kata ya Ngokolo mjini Shinyanga kulikotokea tukio hilo Sebastian Peter amesema kifo cha God ni mipango ya mungu kutokana na kwamba marehemu hakuwa mgeni wa pombe na kwamba inadaiwa kuwa kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa analalamika kusumbuliwa na vichomi siku hiyo.
Akizumgumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa alikiri kuupokea mwili wa marehemu muda wa saa moja jioni Desemba 25 mwaka huu,akiwa tayari amefariki dunia na kesho yake Desemba 26 ndugu wa marehemu walifika hospitalini hapo na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi hivyo kushindwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema bado hajapata taarifa kuhusu tukio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu na marehemu anayejulikana kwa jina la John ameuambia mtandao huu kuwa tayari mwili wa marehemu God Shaini umesafirishwa kwa ajili ya mazishi hapo kesho nyumbani kwa mama yake Mabatini mkoani Mwanza.
Social Plugin